Deuteronomy 29:1-3

Kufanya Upya Agano

1 aHaya ndiyo maneno ya Agano Bwana aliyomwagiza Musa kufanya na Waisraeli huko Moabu, kuwa nyongeza ya Agano alilofanya nao huko Horebu.

2 bMusa akawaita Waisraeli wote akawaambia:

Macho yenu yameona yale yote Bwana aliyofanya kwa Mfalme Farao huko Misri, kwa maafisa wake wote na kwa nchi yake yote.
3 cKwa macho yenu wenyewe mliona yale majaribu makubwa, ishara zile za miujiza na maajabu makubwa.
Copyright information for SwhKC